Kiswahili-Swahili

Best Meditation Method in Kiswahili-Swahili

Mazoezi ya GSSY

Ni kitu gani mazoezi ya mwili na akili (Yoga) ya Guru Siyag (GSSY) yanahusisha?

Mazoezi ya GSSY yanahusisha kurudia kuimba (kurudia akilini) maneno ya sala ya kiungu na kutafakari. Guru Siyag humwingiza mwombaji  katika GSSY kama mfuasi wake kwa kumpa neno la sala ya kiungu  — kulirudia kimyakimya muda wote wa saa na pia humfundisha mbinu ya kutafakari. Kurudia kuimba (Japa) neno la sala ya kiungu kunakuwa bila hiari wakati kunaporudiwa mara kwa mara muda wote kwa kipindi cha muda fulani. Hata hivyo hii inategemea moja kwa moja na kiasi cha bidii, imani na usafi ambao kurudia kuimba kunafanyika. Katika hali fulani kurudia kutamka/kuimba kunafanyika bila hiari baada ya zaidi ya wiki tu ya mazoezi wakati katika mazingira mengine inachukua wiki mbili au hata miezi michache. Licha ya kurudiarudia kuimba maneno ya sala ya kiungu (mantra), mfuasi anatakiwa pia kutafakari kwa dakika 15 kila mara, mara mbili au tatu kwa siku.

Utaratibu wa hatua kwa hatua wa kutafakari chini ya GSSY

  • Kaa katika mkao wa kutulia.
  • Unaweza kukaa kwa kukunja miguu sakafuni, lala chini, kaa kwenye kiti / kochi n.k., ili kutafakari.
  • Angalia picha Guru Siyag kwa dakika moja au mbili hadi ukumbuke picha.
  • Kisha funga macho yako na zungumza kimykimya kwa Guru Siyag, “Nisaidie kutafakari kwa dakika 15.”
  • Kisha, na macho yako yakiwa bado yamefumbwa, fikiria picha ya Guru Siyag kati sehemu kati ya nyusi zako (pia inajulikana kama jicho la tatu). Hii ina maana kwamba unatakiwa ujaribu kufikiria picha ya Guru Siyag katika akili yako katika sehemu ya paji la uso.
  • Wakati unafikiria picha, rudia kimyakimya (kuimba) kwa dakika 15 mantra (maneno ya sala ya imani) iliyotolewa na Guru Siyag. (Angalia ‘Jinsi ya kupokea Mantra)
  • Wakati wa kutafakari, unaweza kuona mikao ya yoga ya ghafla bila hiari au mishtuko. Kuyumba, kutikisika kichwa, kucheza kichwa kwa kasi kutoka kushoto kwenda kulia na kushoto tena, kutanuka/kujaa hewa na kunywea kwa tumbo, kupiga makofi, kuunguruma, kunung’unika au kucheka kunaweza kutokea mara nyingi. Usipaniki wala kuwa na wasiwasi.  Hatua hizi zinatokea ghafla bila kutaka, zimepangwa na nguvu ya Mungu Kundalini, na zinahitajika kwa ajili ya kukutakasa ndani na kukuweka tayari kwa ajili ya hatua zaidi nyingine.
  • Unaweza pia kuona mitetemo, kuona mwanga mkali, rangi au hata kuwa na maono au ishara za siku za nyuma na matukio ya baadaye. Hizi ni dalili kwamba unaendelea vizuri katika njia ya kiroho.
  • Hata hivyo, hata kama hauoni mikao yoyote ya yoga au hauoni maono, haimaanishi kwamba hauendelei. Kwa uwezekano wote, nguvu ya Mungu iliyoamshwa ndani yako labda imeamua kwamba hauhitaji hali hizi.
  • Utaona kwamba kutafakari kwako kutafikia mwisho hasa utakapofikia kikomo cha wakati uliokuwa umeweka awali.

Jinsi ya kupokea sala/maneno ya imani (mantra) ya dikshā

http://gurusiyag.org/online-initiationshaktipat-diksha/

Faida za GSSY

Faida Muhimu za GSSY

Kutafakari kwa GSSY na kurudia muda wote maneno ya sala ya kiungu yaani mantra yaliyotolewa na Guru Siyag huleta mabadiliko yafuatayo katika maisha ya mwombaji:

  • Uhuru kutoka kila aina ya magonjwa ya kimwili ikiwa ni pamoja na VVU / UKIMWI, kansa, Pumu, shinikizo-la-damu la juu au chini, maumivu ya viungo, Kisukari, Spondilitisi, Himofilia, Unene kupita kiasi, maradhi ya moyo, Kiharusi cha kupooza, magonjwa ya ngozi, nk.
  • Uhuru kutoka ulevi kwa aina yoyote ya madawa ya kulevya na vitu, pombe, sigara, kutafuna tumbaku n.k. GSSY pia humwondoa mwombaji kutoka katika utegemezi hatarishi wa chakula.
  • Uhuru kutoka katika ugonjwa wa sononeko la moyo, kukosa usingizi, msongo na magonjwa mengine ya kisaikolojia.
  • Uhuru kutokana na matatizo yanayohusiana na mambo ya kifamilia, kazi, ndoa, elimu, fedha n.k.
  • Uhuru kutokana na athari za Voodoo, uchawi mbaya na mila za dini za kiasia za tafakari.
  • Manufaa kwa wanafunzi ni kwa vile GSSY husababisha ongezeko mbalimbali katika kushika na kuhifadhi, na uwezo kufuatilia au kuzingatia kwa kuweka akili juu ya kitu chochote kinachotakiwa au somo fulani.

Uponyaji wa Magonjwa ya Kimwili.

Magonjwa ambayo binadamu wanakabiliwa nayo yameanishwa na sayansi ya matibabu ya kisasa katika makundi mawili mapana — kimwili na kiakili.  Haya yanatibiwa na madawa ya ndani ya mwili na /au madawa ya nje ya mwili au matumizi ya elimu ya matibabu. Wahenga wa kale wa India walizama kwa kina katika siri za maisha kwa kutafakari na kujifunza kwamba magonjwa hayasababishwi na kukaa kwa bahati mbaya katika wadudu au vimelea, kama wanasayansi wa matibabu wanavyoamini.  Walijifunza kwamba sehemu kubwa ya mateso ya binadamu kwa kweli yanasababishwa na matendo ya kila mmoja katika maisha yake ya zamani.  Kila hatua – nzuri au mbaya – inasababisha msuguano katika mzunguko huo wa maisha au unapelekwa kwa hatua nyingine. Kwa sababu kila mtu ananaswa katika mzunguko usio na mwisho wa maisha na kifo, akiugua magonjwa na kupitia kupanda na kushuka kwa maisha yanayoendelea bila kukoma. Kwa maneno mengine, Sheria ya Kiroho ya Karma – matendo ya siku za nyuma yanasababisha magonjwa na aina nyingine za mateso katika maisha ya sasa – yakiongoza kuwapo kwa binadamu, maisha baada ya maisha katika mzunguko usioisha kamwe.

Katika makala yake ‘Yoga Sutra’, mhenga Mhindi Patanjali alianisha magonjwa katika makundi matatu – Kimwili (Ādhidehik), Kiakili (Ādhibhautik) na ya Kiroho (Ādhidaivik).  Ugonjwa wa Kiroho unahitaji tiba ya kiroho.  Mazoezi ya mara kwa mara ya yoga pekee chini ya uongozi wa Bwana wa kiroho kama Guru Siyag yanaweza kumsaidia mwombaji kupata dawa ya kiroho kwa mateso yake. Mazoezi ya GSSY husaidia mfuasi kukata kwa njia ya mtandao wa Karmic siku za nyuma, kujikwamua na magonjwa na kutambua madhumuni ya kweli ya maisha yake kupitia utambuzi wa kibinafsi (Atma sākshātkār).

Masuala ya Kiroho ya GSSY:

  1. GSSY inatokana na Ashtanga yaani falsafa ya (viungo vinane/miguu minane) ya Yoga kama ilivyopangiliwa na Sage Patanjali katika Yoga Sutra. Mazoezi ya GSSY hupelekea katika utambuzi rahisi usiohitaji nguvu wa viungo hivi vinane.
  2. Baada ya mazoezi endelevu, uimbaji wa mantra (marudio akilini) unakuwa/unafanyika wenyewe bila hiari. Hali hii hujulikana kama Ajapā Japa. Katika hali hii, mwombaji/mtendaji anaona kuwa mantra yaani maneno ya sala ya kiungu yanaimbwa bila ukomo ndani ya yake yenyewe bila hiari yake mwenyewe, bila yeye kuamua kwa upande wa mwombaji/mtendaji.
  3. Wakati mwombaji anapoimba maneno haya ya sala ya kiungu ya mantra bila kuchoka (au anapoona Ajapā Japa), yanajibadili yenyewe kuwa katika sauti ya kiungu. Hii inajulikana kama Anhad Nada.  Sauti halisi ya umbo inatengenezwa wakati kitu kimoja kinapogonga kingine.  Hii sauti ya mbinguni haina asili hiyo ya umbo; haigongwi,  ni sauti isiyokoma ambayo inaenea ulimwengu mzima.  Nad inasikiwa na mwombaji katika moja ya masikio yake, na ni dalili ya mwombaji kuvuka kizingiti kikuu cha hatua za kiroho.
  4. Kwa njia ya mazoezi ya GSSY, mwombaji anapata nguvu nyingi za kiungu. Moja ya nguvu hizi za kiungu inajulikana kama Prātibh Gyāna (Maarifa ya kung’amua bila kufikiri sana).  Wakati maarifa haya yanapopatikana, mwombaji anaweza kutabiri na kusikia matukio ya siku zijazo yasiyo na ukomo na pia ana maono ya siku za nyuma.
  5. Wakati wa kutafakari, waombaji wanaweza kuona Khechri Mudra, mkao wa kiYoga ambapo ulimi unavutwa nyuma na unachoma sehemu ya juu ya kinywa ambayo inatoa Amrit, nekta/asali ya miungu, ambayo ni dawa ya maji ya maisha uishi muda mrefu ukiwa kijana. Amrit inaimarisha kinga ya mwili na inamwondoa mwombaji katika magonjwa yasiyotibika.
  6. Mazoezi ya GSSY huleta mabadiliko katika Vrittis (tabia za ndani) za mwombaji kutoka Tāmasic (giza, kuzubaa, uzembe) kwenda Rājasic (shauku, kuchangamka) ili kuwa Sāttavic (mwenye bidii, msafi, mwelewa). Mabadiliko katika Vrittis kimsingi yana maana ya mabadiliko kwa ujumla katika nafsi/utu wa mwombaji.
  7. Mwombaji hatimaye anafikia hatua ya Moksha (uhuru wa kutoka katika mzunguko wa maisha na kifo) na mabadiliko ya kiungu.

Kuondokana na Msongo

Sayansi ya Tiba inatibu msongo kwa madawa ya kuzoelea/kulevya (dawa za kutuliza kwa kulala, vidonge vya usingizi, dawa za kuzuia hali fulani n.k.) ambazo kwa nadra zina uwezo wa kutibu mgonjwa.  GSSY pia inaona ulevi kama tiba lakini ni aina ya kulevya Ananda (furaha au neema) inayoletwa na kuimba mara kwa mara kwa maneno ya sala ya kiungu yaani mantra ya Guru Siyag.  Wahenga wameelezea neema hii ya kiungu kama “ulevi bila madawa ya kulevya.” Ananda humwondoa mwombaji katika msongo na magonjwa yanayohusiana na msongo kama vile huzuni, shinikizo la damu, kukosa usingizi, hofu ya kitu, n.k. kwa siku chache tu.

Kuondokana na Kuzoelea Madawa ya Kulevya

Kila mtu ana tabia tatu za asili: Sāttavic (safi, nyepesi), Rajasic (shauku) na Tamasic (kuzubaa, uzembe).  Tabia hizi huamua si tu kupona kwa jumla kwa akili ya mtu, mtazamo juu ya maisha na matendo, bali pia upendeleo wake wa mlo au au uchaguzi wa vyakula na vinywaji atakavyotumia. Mazoezi ya mara kwa mara ya GSSY huwezesha utawala wa Sāttavic kuliko Rājasic na tabia za Tāmasic , na hivyo kusababisha mabadiliko yanayohusiana na tabia mbili zinazofuatia.  Utawala kwa ubora wa Sattvic kwa upande mwingine huleta mwelekeo wa tabia za mtu za ndani kuelekea matendo mazuri ya ufahamu, akili na kufikiria kwa sahihi. Ndivyo inavyokuwa pia kwa upendeleo wake wa chakula na vinywaji.  Matokeo ya jumla ya mabadiliko haya ni kwamba chochote ambacho ni kibaya na chenye madhara kwa ustawi wa mwili na akili ya mtu na mageuzi ya kiroho humuacha kwa hiari yake mwenyewe bila juhudi ya ufahamu wa mtu kufanya hili kutokea.  Hivyo, kama mtu anasumbuliwa na ulevi wa madawa, pombe au kuvuta sigara, ulevi au kuzoelea madawa kutamwacha au kama anapendelea aina ya chakula ambacho kina madhara kwa afya yake, atapiga hatua ya kukichukia taratibu na kurejea kwenye maamuzi mazuri ya kiafya kwa sababu ya mabadiliko katika sifa na tabia yake ya ndani kulikoletwa na kuiimba kwa mantra na kutafakari. Swami Vivekanand amesema kuhusu kuondokana huku kwenyewe kwa ulevi, “Huhitaji kuacha/kuondokana na vitu; vitu vyenyewe vitakuacha/vitaondokana nawe.

Upekee wa Yoga Guru Siyag.

  1. Mazoezi ya GSSY hayahusisha mila, matendo ya taratibu za ibada, desturi na sadaka (nazi, ubani, maua n.k.).
  2. Mtafutaji/Mwombaji katika sehemu yoyote ya dunia anaweza kuona tafakari ya kina kwa kutafakari tu kwenye picha ya Guru Siyag.
  3. Guru Siyag hasisitizi kwa waombaji kukutana naye ana kwa ana kwa ufundwaji/kufunzwa.
  4. Uanzishwaji kitu/Kufundwa kwa GSSY kupitia video/audio CD, matangazo ya TV au kipande cha video kwa barua pepe ni fanisi/inatosha kama ilivyo katika uanzishwaji/ufundjwaji wa mtu.
  5. Kama mwombaji/mtafuta msaada anashindwa kwa sababu fulani (mtendaji ni mtoto mdogo au akiwa hana fahamu au mlevu kiakili) kuimba sala ya Guru Siyag na kufanya tafakari,  jamaa au rafiki yeyote wa karibu aliyefundwa anaweza kuimba na kufanya taratibu kwa niaba yake.
  6. Guru Siyag hatoi kozi au hafanyi madarasa yoyote kwa Yoga.
  7. GSSY ni bure kabisa bila gharama.
  8. Hakuna usajili unaohitajika kwa ajili ya GSSY.
  9. Guru Siyag haombi zawadi ya fedha au za aina hiyo kutoka wanaotafuta kufundwa GSSY.
  10. Hakuna milo maalum au vikwazo vya mitindo mingine ya maisha chini ya GSSY.
  11. Guru Siyag hazuii wafuasi wake kufuata taratibu zingine za Gurus baada ya kufundwa/kufunzwa.
  12. Guru Siyag hatoi mahubiri ya kidini. Yeye anaelezea tu falsafa ya GSSY.
  13. Guru Siyag hauzi /hatoi dawa, dawa za mimea, tiba mizizi au bidhaa ya aina yoyote.
  14. Waombaji wa rangi yoyote, dini, utaifa, tabaka, imani au jinsia yoyote wanakaribishwa katika jamii ya GSSY.

Uamshaji wa Kundalini

Kurudiarudia kuimba na kutafakari pamoja kunamuamsha Kundalini.  Kundalini ni nguvu ya mungu wa kike ambayo imelala tuli katika namna isiyoonekana chini ya uti wa mgongo katika mwili wa binadamu.   Ameunganishwa kwenye viungo sita vya nguvu isiyoonekana iitwayo Chakras iliyowekwa juu ya nyingine katika uti wa mgongo.  Wakati Siddha Guru (Bwana mkamilifu) kama vile Guru Siyag anapomuamsha Kundalini kwa kutoa Shaktipāta (kumpa nguvu ya kiroho) kwa sala yake ya kiungu, anajitokeza kupitia chakras sita na hatimaye anafikia Sahasrara, sehemu katika taji la kichwa, ambapo Mungu anakaa.   Kundalini aliyeamshwa hutakasa mwili mzima wa mwombaji kwa kuleta āsanans za bila hiari za yoga kriyās, bandhs, mudras, Pranayam na kadhalika wakati wa kutafakari.  Mwombaji hawezi kuanzisha au kusitisha mihemko hii ya Yoga kwa hiari na akili yake mwenyewe. Hizi Kriyās humwondoa mwombaji kutoka katika taabu za mwili na akili, ulevi, na humtia katika Moksha kwa kumweka katika njia ya mabadiliko ya kiroho.